VIDEO: Kanye West Atoa Mpya...Aitupa TUZO ya Grammy Chooni na Kuikojolea Haja Ndogo

Kanye West ameitupa chooni tuzo ya Grammy na kuikojolea, tuzo ambayo ni ndoto ya kila msanii duniani kuja angalau kuishika tu kwa mikono yake. Kanye anafanya hivi ikiwa ni muendelezo wake wa kutilia mkazo madai yake ya uonevu na utumwa wanaofanyiwa wasanii kwenye label za muziki na makampuni.

Wiki hii Kanye amekuwa akipazia sauti suala hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kuzitupia lawana label za Sony na Universal, Ye amefikia hatua ya kutaka kununua haki zote za kazi zake yaani Master Recordings toka kwenye label hizo.

Kanye ni mshindi mara 21 wa tuzo za Grammy, akiwa miongoni mwa wasanii walioshinda mara nyingi zaidi. VIDEO:

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments