9/10/2020

Video: Majambazi Waliovamia Kibanda cha M-Pesa Wauawa kwa Kupigwa Mawe

 
Watu wawili wanaodaiwa kuwa ni Majambazi wameuawa kwa kupigwa mawe na wananchi baada ya majambazi hao kuvamia duka la M-Pesa na kufyatua baruti hewani kisha kumshambulia kwa kumpiga mabapa ya panga mmiliki wa kibanda cha M-Pesa na kupora shilingi Milioni 1.7 Mjini Kahama mkoani Shinyanga.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea September 8,2020 majira ya saa mbili na nusu usiku katika eneo la Manzese, Kata ya Busoka, Tarafa ya Kahama Mjini, Wilaya ya Kahama na Mkoa wa Shinyanga.


“Majambazi wawili ambao bado hawajafahamika majina wala makazi yao, umri kati ya miaka 25-30, waliuawa kwa kurushiwa mawe na wananchi wa eneo la Manzese Mjini Kahama baada ya majambazi hao kuvamia duka la M-pesa na kufyatua baruti hewani kisha kumshambulia kwa kumpiga mabapa ya panga mgongoni mmiliki wa kibanda cha M-pesa aitwaye Paulo Charles Inena (32), mfanyabiashara mkazi wa Lugela kwa lengo la kumnyang’anya pesa za mauzo” Kamanda Magiligimba


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger