Vifurushi 21 vya msaada wa Jack Ma 'havikufika' KenyaMisaada kutoka kwa Jack Ma kwa ajili ya kukabiliana na coronaImage caption: Misaada kutoka kwa Jack Ma kwa ajili ya kukabiliana na corona

Naibu wa waziri wa uchukuzi wa Kenya, Chris Obure amefichua kuwa vifurushi 21 vilivyokuwa na vifaa vya matibabu vilivyotolewa na wakfu wa Jack Ma mwezi Machi kama msaada wa kukabiliana na Covid 19 haikufika Kenya.


Bwana Obure alisema hayo siku ya Alhamisi mbele ya kamati ya bunge ya afya japo hakudokeza ni vifaa vya aina gani vilikuwa ndani ya vifurushi hivyo.


Aliongeza kuwa vifaa hivyo havikuwahi kuwawasili nchini kutoka Ethiopia ambako misaada ya Jack Ma katika eneo hilo ilitumwa kwa ajili ya kusambazwa katika nchi zingine.


Wizara ya uchukuzi iligundua kuwa vifurushi 21 havikuwepo baada ya kuthibitisha hilo katika stakabadhi za kuegesha kutoka China.‘’Binafsi niliongea na maafisa wakuu wa Wizara ya Afya na walinithibitishia kuwa wanafuatilia suala hilo’’ alisema bwana Obure.


Kumekuwa na madai kwamba misaada ya Covid-19, ikiwemo ile kutoka kwa Ma ilitumiwa vibaya au kutoweka katika njia za kutatanisha.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments