Wafungwa Zaidi ya 200 Watoroka Gerezani Uganda...Wakimbilia Mlimani..

 


ZAIDI ya wafungwa 200 wa Gereza la Singila, Moroto Kaskazini Mashariki mwa Uganda, wametoroka gerezani baada ya kufanikiwa kumuua askari mmoja katika majibizano makali ya risasi.

 

Kamishna wa Magereza nchini Uganda, Johnson Byabashaija, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba wafungwa hao waliwazidi nguvu askari magereza na kufanikiwa kuvunja ghala la silaha ambapo waliiba bunduki 15 walizozitumia kufanikisha kutoroka kwao.

 

Byabashaija amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea na msako mkali kwenye Mlima Moroto walikotorokea wafungwa hao.

That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments