9/16/2020

Wakala wa Kagere amtolea uvivu kocha wa Simba “Kocha huyo angejua kilichomtokea mwenzake”Wakala wa mchezaji wa Simba SC Meddie Kagere anayefahamika kwa jina la Patrick Gakumba ameeleza kuwa kocha wa Simba SC Sven Vandenbroeck kuwa aulize kocha wa zamani wa Gor Mahia kutokea Brazil naye alikuwa hampangi Kagere.

“Timu ya mashabiki timu sio ya kocha muda utaongea sifa za mshambuliaji bora mara mbili alikuwa Top Scorer Rwanda, Kenya na Tanzania amekuwa mfungaji bora mara mbili pia wa SportPesa, uwezo wa Meddie huko pale pale mashabiki wanajua na muda utaongea lakini mwalimu asiyempa nafasi janja janja zinazofanywa ili kumpoteza kwenye ramani tunajua “>>>Patrick Gakumba

Meddie Kagere kwa sasa amekuwa hapati nafasi sana ya kucheza chini ya kocha wa Simba SC Sven Vandenbroeck licha ya kuwa ndio mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania bara kwa msimu uliomalizika, kitu ambacho kinaleta maswali miongoni mwa mashabiki kutokana na mfungaji bora wa timu kukaa benchi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger