9/23/2020

Wakenya Ruksa Kushiriki Maziko ya Waliokufa kwa CoronaRAIA wa Kenya kuanzia sasa wameruhusiwa kushiriki katika shughuli za mazishi ya wapendwa wao waliofariki kutokana na virusi vya corona baada ya serikali kulegeza masharti tofauti na awali ambapo walipiga marufuku.


Awali, ndugu wa karibu wa mtu aliyekufa kwa corona hawakuruhusiwa kufanya chochote zaidi ya kuangalia kwa mbali wakati maafisa wa afya waliojihami kwa mavazi maalum wakifanya shughuli za maziko.

Maafisa wa afya wamesema kuwa miili ya waliokufa kutokana na maambukizi ya virusi vya corona haiwezi kuambukiza virusi hivyo.

Shirika la afya duniani (WHO) na kituo cha kudhibiti magonjwa Afrika (CDC) hawajasema bado kama maiti haiwezi kuambukiza Covid-19, lakini wamebadilisha utaratibu na kuruhusu familia kuaga wapendwa wao.


Nchini Kenya, maofisa wa afya watakuwepo katika maziko ili kutoa mwongozo na kuhakikisha usalama unazingatiwa.


“Tutaruhusu shughuli zote za mazishi za kidini na kitamaduni kufuatwa kulingana na tamaduni za marehemu,” serikali ilisema na kukiri kuwa zuio waliloliweka mwezi uliopita lilikuwa gumu kufuatwa.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger