9/24/2020

Wanafunzi Wenye Ueleo Hafifu Kuundiwa Mpango MaalumShule ya sekondari ya St Mark’s iliyopo Kongowe, Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam, imeandaa mkakati  wa  kuwatambua wanafunzi  walio chini kiuwezo na kuwasaidia ili nao waweze kufanya vizuri katika masomo yao.


Akizungumza wakati wa mahafali ya kidato cha nne mwalimu mkuu wa shule hiyo, Leticia Joseph amesema.


“Tunatambua  baadhi  ya wanafunzi wanakuwa chini kiuwezo darasani baada ya kubaini hilo shule imeandaa  mkakati ambapo wanafunzi wasio na uwezo wanatambuliwa  na kusaidiwa ili waweze kuinuka kielimu,”amesema.


Ameendelea kusema kuwa shule yao imekuwa na mafanikio makubwa katika ufaulu na hali hiyo kuifanya shule hiyo kuwa na matokeo mazuri kila mwaka ambapo kidato cha nne katika mitihani ya mwisho wanafaulu na kujiunga na kidato cha tano na wengine kujiunga vyuo.


“Mafanikio  haya yanatokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya walimu na wanafunzi katika masomo yanayotolewa na mafanikio mengine ambayo shule imekuwa ikiyapata kutokana na  kufanya mitihani vizuri ni uwepo wa walimu wa wa kutosha, maabara zenye vifaa vya kutosha, maktaba yenye vifaa vya kujifunzia.


“Shule imewalea kimaadili wanafunzi hivyo mkitoka shule  mkirudi nyumbani msijiingize  katika Mambo yasiyofaa  mnatakiwa kuyaendeleza yale mliyoyapata shuleni.” alimaliza kusema.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger