9/06/2020

Wanajeshi Wawili wa Ufaransa Wauawa Katika Shambulizi MaliWanajeshi wawili wa Ufaransa wameuawa nchini Mali, baada ya shambulizi la mlipuko dhidi ya gari lao la kijeshi. Ofisi ya Rais Emmanuel Macron imesema hayo usiku wa kuamkia leo, na kuongeza kwamba gari hilo pia liliharibiwa kufuatia shambulizi hilo lililotokea Tessalit, kaskazini mwa Mali.

Macron amesema wanajeshi hao wameuawa wakati wa vita dhidi ya ugaidi katika eneo linalokumbwa na machafuko la Sahel.

Ufaransa inashiriki mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi yaliyomo eneo hilo la Sahel. Baadhi ya makundi hayo yanashirikiana na kundi linalojiiza Dola la Kiislamu IS pamoja na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda. Takriban wanajeshi 5,100 wa Ufaransa ni sehemu ya ujumbe wake uitwao Barkhane.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger