9/07/2020

Wasanii Lulu Diva, Belle 9 na Bonge la Nyau Wamepata Ajali ya Gari

Wasanii wa Bongofleva Lulu Diva, Belle 9 na Bonge la Nyau wamepata ajali ya gari alfajiri ya leo Chalinze Pwani wakiwa safarini kuelekea Dar es salaam.

Lulu Diva ambae ameongea na simu kwa tabu amethibisha taarifa hizo kwa kusema ‘Ni kweli Millard tumepata ajali Chalinze, tulikua tunaendeshwa, mimi nimeumia kichwani nimevimba ila Belle 9 kaumia zaidi jamani amewaishwa Hospitali, @bongelanyau kaumia ila kiasi... mimi niko Polisi kuchukua Pf3 kisha nimfate @belle9tz Hospitali” @luludivatz

“Sijui chanzo ni nini maana wakati ajali inatokea nilikua nimelala nikaja kushtukia gari imeacha barabara na kupinduka, Belle 9 anaonekana ameumia mgongo na kichwani” - Lulu Diva.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger