9/24/2020

Wasanii wanne wakike wanao ng’aa kwasasa nchini Kenya!Kwasasa anatamba na ngoma inayojulikana kama, Jipe aliyomshirikisha msanii nyota Marioo kutoka hapa Tanzania. Nadia anashukiwa kua ndiyenmsanii wakike anayeingiza mkwacha mrefu zaidi nchini Kenya kuliko wengine na kwa upande mwingine ametokea kua ndie staa wakike ambae anafanya colabo nyingi na mastaa wakiume nchini Kenya wenye hadhi ya A list. Wakiwemo Willy Paul, Khaligraph Jones na wengineo.


Na kunatetesi hivi majuzi alishaajiri muandishi wa nyimbo zake kutoka Tanzania na anamlipa mtonyo mrefu na kumkodia nyumba kwenye mtaa wakifahari wa Lavington jijini Nairobi Kenya.


2. JovialKwasasa anatamba na ngoma inayoitwa pakua, ambayo amemshirikisha rapper mkali wa nchini Kenya maarufu kama Mejja. Jovial awali alishawahi kusajiliwa na msanii nyota nchini Kenya Otile Brown lakini akajitoa baade miezi mitatu huku tetesi za chini ya kapeti ziki nadi kua makubaliano yao upande wa mahusiano yalivunjika baada ya Otile kuzidisha matakwa kupita mipaka nahivyo Jovial kwa kukwepa lawama akaona ajitoe kirahisi siku chache baada ya kuzawadiwa gari la kutembelea na staa huyo wakiume.


3. VivianUnapotaja jina la msanii Vivian nchini Kenya kwasasa, lazima utapata jibu la “Ndio Manake”. Jibu hili linatokana na wimbo wake aliomshirikisha msanii na rapper anaekua kwa kasi Kenya kwajina Steve Simple Boy anaefahamika kwa wimbo wake wa ” Vijanaa tuache mihadarati”. Vivian amefanya kazi nyingi na mastaa tofauti wa Kenya na hata nje akiwemo Jose Chameleon gwiji wa muziki kutoka Uganda.


4. AdasaNi msanii ambae mashabiki wa muziki nchini Kenya wamemuelewa kwa mda chache sana. Hii inatokana na jinsi msanii huyu alivyobarikiwa na sauti tamu yenye uwezo wakumtoa nyoka pangoni. Adasa kwasasa anatamba na kibao “Tujikakamue” alichoshirikishwa na staa na rapper Benzema wa nchini Kenya. Kibao ambacho kimewafanya mstaa wakubwa wa muziki nchini Kenya kufunguka na kumsifia sana Adasa. Huku rapper mkali siwa nchini Kenya pekee bali Africa nzima Khaligraph Jones kuamua kumu pandisha kwenye mtandao wake wa instagram na kumusifia kwa sifa kedekede.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger