Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Watu wanne wakamatwa nchini Ubelgiji baada ya kutekwa nyara kwa helikopta

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREMaafisa wa polisi nchini Ubelgiji leo wamewakamata washukiwa wanne wanaoaminika kuiteka nyara helikopta moja na kumlazimisha rubani wake kuirusha ndege hiyo juu ya majengo mawili ya magereza katika jaribio linaloaminika kuwa la kuwatorosha wafungwa. 

Hakuna habari zaidi zilizotolewa kuhusiana na washukiwa hao.Ripoti za awali zinaashiria kuwa maafisa wa polisi wanawasaka watu watatu. 

Kikimnukuu mwendesha mashtaka wa umma katika mji wa Kaskazini wa Antwerp, kituo cha habari cha Belga kimeripoti kuwa washambuliaji walichukuwa udhibiti wa ndege hiyo mjini humo siku ya Ijumaa. Kwa mujibu wa waendesha mashtaka, washukiwa hao walikuwa na miadi na safari ya helikopta hiyo iliyokuwa ianzie safari yake mjini Antwerp. 

Kituo cha habari cha VRT kimeripoti kuwa polisi wanaamini watu hao walitaka kutua na kuwatorosha wafungwa kutoka gerezani lakini helikopta hiyo haikuweza kutua katika uwanja wa gereza hilo kwasababu ya ukubwa wake.

Post a Comment

0 Comments