9/28/2020

Wema Sepetu Ajipunguzia Umri, Sikuzaliwa 1988MALKIA wa Bongo Movies, Wema Sepetu,  amekiri kutoa taarifa zisizo za kweli kuhusu  mwaka wa kuzaliwa kwake na umri wake.

Wema ambaye leo Septemba 28, ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, ameeleza kuwa si kweli kwamba alizaliwa mwaka 1988 bali ukweli ni kwamba alizaliwa mwaka 1990,  hivyo mwaka huu ametimiza umri wa miaka 30.

Katika maelezo yake kwenye ukurasa wake wa Instagram, Wema alikiri na kuweka wazi kuwa awali alitoa taarifa zisizo za kweli kuhusu mwaka wa kuzaliwa kwake. Hata hivyo taarifa za mwaka wa kuzaliwa kwake hasa mtandaoni zilionyesha kuwa ni mzaliwa wa Septemba 28, 1988.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger