9/30/2020

Willow Smith Ampongeza Mama Yake Kuchepuka na August Alsina#GetToKnow Miongoni mwa stori zilizokamata vichwa vya habari duniani mwaka huu ni hii ya mke wa Will Smith, Jada Pinkett kuanika wazi mahusiano yake na August Alsina.


Wengi walipata nafasi ya kujadili suala hili, ikiwemo Will Smith mwenyewe ambaye alikaa kitako na Jada kujadili. Sasa jana ilikuwa nafasi ya kupata mawazo kutoka kwa familia yake ambapo binti yake Jada, Willow Smith amefunguka kuhusu mahusiano hayo ya Mama yake mzazi.


Kupitia kipindi cha Red Table Talk jana Jumatatu ambacho kilimuhusisha pia Bibi yake Willow, kilimshuhudia Willow Smith (19) akipongeza uamuzi huo wa mama yake kuwa na mahusiano na August Alsina licha ya kuwa kwenye ndoa na baba yake, Will Smith.

-

"Ninataka kuiweka hii mezani. Ninajivunia wewe sana. Kuwaona wewe na Baba mkifanya makubaliano haya, kwa ajili yangu, hii niliichukulia kama 'Sawa, huo ndio mpango sahihi sasa.' huo ndio upendo wa kweli." alikazia Willow.


Jada na Will Smith walifunga ndoa mwaka 1997, lakini katika kipindi cha hivi karibuni wamekuwa kwenye ndoa ya wazi (Open marriage) ambayo iliwaruhusu kila mmoja kutafuta mwenza wa kumliwaza, hii ni baada ya kupitia mfarakano na kutoelewana hivyo kuamua kupeana nafasi ya kila mmoja kufanya mambo yake.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger