9/25/2020

Wizara ya sheria yataka kupigwa marufuku mara moja kwa WeChat MarekaniWizara ya sheria nchini Marekani inataka kupigwa marufuku mara moja upakuaji wa app ya WeChat kupitia kampuni za Apple na Google, ikisema huduma hizo za kutuma ujumbe zinazomilikiwa na makampuni ya China ni kitisho kwa usalama wa Marekani. 

Wiki iliyopita wizara ya biashara ya Marekani ilichukua hatua ya kupiga marufuku WeChat kutoka katika hifadhi za app za Marekani lakini siku ya Jumamosi, jaji wa mahakama Laurel Beeler jimboni Califonia alikubali kuchelewesha vizuwizi hivyo vya Marekani, akisema vitaathiri haki za watumiaji. 


Katika kesi hiyo leo, wizara ya sheria imemtaka Beeler kuruhusu upigwaji marufuku mara moja wakati kesi hiyo ikiendelea kufanyiwa kazi katika mahakama.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger