9/20/2020

Yanga Kama inanawa Vile..Mwendo Mdundo tu

 


Mabingwa wa kihistoria  wa Tanzania Yanga sc imeibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya wakata miwa wa Kagera sugar .


Shukrani za dhati kwa mchezaji toka nchini DRC MukokoTonombe  ambae dakika ya 71 alipeleka kilio kwa wapinzani wao Kagera sukari .


Yanga  imefanikiwa kupata ushindi wao wapili mfululizo katika ligi kuu ya soka Tanzania bara baada ya kuifunga timu ya Kagera sugar mchezo uliopigwa dimba la kaitaba mjini bukoba


Nahodha wa Yanga Deus kaseke amesema wamecheza na timu nzuri na timu hiyo ilikosa Bahati huku wao wakitumia nafasi waliyopata.


Ushindi huo ni wa sita mfululizo kwa Yanga dhidi ya Kagera katika Uwanja wa Kaitaba kama ambavyo reodi zinavyoonyesha tangu msimu wa 2015/16.


Yanga sc sasa inaongoza ligi baada ya kufikisha jumla ya pointi 7 baada ya kushuka dimbani mara 3 huku wakitarajia kucheza wiki ijayo dhidi ya Mtibwa sugar katika dimba Jamhuri Mjini Morogoro.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger