9/27/2020

Yanga Waichapa Mtibwa Sugar Ligi KuuYanga SC wameendeleza staili yao ya ushindi mwembamba katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya leo pia kuichapa Mtibwa Sugar 1-0 Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.


Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, beki Mghana, Lamine Moro aliyeunganisha kwa mguu wa kulia kona ya chini chini ya kiungo Muangola, Carlos Carlinhos dakika ya 61.


Na kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 10, sawa na mabingwa watetezi, Simba SC ambao wanaendelea kukaa nafasi ya pili kwa faida ya mabao mengi waliovuna baada ya mechi nne za awali.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger