Zahera aipiga mkwara Simba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



 Mtendaji mkuu wa Klabu ya Gwambina ya jijini Mwanza, Mwinyi Zahera amesema mechi yao dhidi Simba chochote kinaweza kikatokea kwakuwa Simba ni timu kubwa nchini lakini kikosi chake kipo tayari kukabiliana nao siku ya Jumamosi Uwanja wa Benjamini Mkapa Dar Es Salaam.

 Zahera amesema pamoja na ubora wa kikosi cha Simba pamoja na kuwa na wachezaji wenye viwango vikubwa nchini lakini kamwe hawezi kutishika na ukubwa huo.


"Mimi nimeshacheza na Sadio Mane, Mohamed Salah lakini sikuwaogopa vipi nije kuwaogopa kina Kagere na Chama ingawa ni wachezaji wazuri, nawaheshimu lakini siwezi kuwaogopa" amesema Zahera.


Aidha, Kocha huyo amesema ili waone ukubwa wa Simba basi wawafunge zaidi ya goli nane kwakuwa hata Barcelona waliwahi kufungwa goli nane na Buyern Munich ya Ujerumani katika nusu fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya mwezi Agosti 202


Itakumbukwa Kocha Mwinyi Zahera aliwahi kuifundisha Klabu kongwe nchini Yanga msimu wa 2018-19 na katika msimu wa 2019-20 alifungashiwa virago kikosini humo kutokana na kuwa na muendelezo mbovu wa matokeo katika msimu wake wa mwisho.


Gwambina bado haijawapata ushindi katika michezo mitatu iliyopita ambayo walipata suluhu dhidi ya Kagera Sugar kabla ya kufungwa na Ruvu Shooting na Biashara ya Mara huku ikiwa haijafunga goli hata moja

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad