10/16/2020

Africa ‘haiwezi kuhimili’ wimbi la pili la virusi vya coronaShirika la afya duniani (WHO) limeonya kuwa Afrika haiwezikuhimili wimbi la pili laCovid-19, likisema kuwa litakuwa na athari kubwa hususan za kiuchumi.


Onyo hilo linatolewa wakati maambukizi yakiendelea kuongezeka katika nchi nyingi ambazo zililegeza sheria za kupambana na maambukizi hayo hivi karibuni.


WHO linasema virusihavitaweza kudhibitiwakama mataifa ya Afrika yataendelea kufungua shughuli zakebila kuweka tahadhari za kuzuwia maambukizi ya virusi vya Corona.


Imeonya pia juu ya kurejea kwa vipindi vya amri za kutotoka nje ambazo inasema Afrika haiwezi kuvihimili.


Mkurugenzi wa Who kanda ya Afrika, Matshidiso Moeti, pia amesema hatua zimewekwa kuhakikisha bara hilo linapata sehemu yake ya ya chanjo yoyote inayotengenezwa.


Afrika imeripoti zaidi yavisa milioni 1.6 vya virusi vya corona tangu mlipoko huo ulipoanza huku watu 39,000 wakifa kutokana na maradhi hayo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger