10/24/2020

Al Ahly Watinga Fainali Mabingwa AfrikaKIGOGO wa soka kutoka Morocco, Wydad Casablanca, amekubali kapigika nje-ndani kwenye mtanange wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya bingwa wa kihistoria wa michuano hiyo National Al Ahly ya Misri.


 


Akiwa nyumbani Wydad alitunguliwa 2-0, juma lililopita na usiku wa jana Ahly akaonyesha umwamba akiwa kwenye uwanja wa nyumbani  baada ya kushinda magoli 3-1.


 


Al Ahly wametinga fainali kwa jumla ya ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Wydad na sasa anamsubiri mshindi baina ya Zamalek ambaye anaoongoza mechi ya mkondo wa kwanza kwa ushindi wa  1-0 dhidi ya Raja.  Mtanange huo utachezwa Novemba Mosi, wakati fainali itachezwa Novemba 6 mwaka huu.


 


Haya ni mafanikio ya kocha mpya kutoka Afrika ya Kusini, Pitso Mosimane, ambaye amejiunga na Klabu hiyo hivi karibuni akitokea Mamelodi Sundowns.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger