Alichokisema Magufuli Baada ya Kumpigia Simu Zitto Kabwe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, amempigia simu mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma mjini, Zitto Kabwe, kwa lengo la kumjulia hali na kumtakia heri ili apone haraka, baada ya hapo jana kupata ajali ya gari na kupata majeraha kadhaa.

 

Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 7, 2020, na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa kupitia ukurasa wake wa Twitter.


"Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amempigia simu na kumpa pole Mhe. Zitto Zuberi Kabwe,  aliyepata ajali ya gari jana mkoani Kigoma, amemuombea heri ili apone haraka na pia amewashukuru madaktari na wauguzi wa kituo cha afya cha Kalya na Hospitali ya Maweni kwa matibabu waliyompa", ameandika Msigwa.


Kwa upande wake Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Twitter ameeleza, kwa sasa anaendelea vizuri yeye pamoja na wenzake wanne waliopata ajali hapo jana Oktoba 6, 2020, maeneo ya Kigoma Kusini.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad