Antonio Nugaz Apongezwa Kwa Uchapaji Kazi YangaMchambuzi wa soka wa kituo cha runinga cha Azam TV ambaye pia ni mwandishi, Gift Macha Oktoba 9, 2020 ametoa pongezi  kupitia ukurasa wake wa Insta kwenda kwa Ofisa Muhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz kwa jinsi anavyofanya kazi ya kuisifia timu yake muda wote na hana habari na Simba au Azam FC.

Jana baada ya mechi ya Yanga na Mwadui iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex ambapo Yanga ilishinda bao 1-0, Nugaz alisema kuwa ataendelea kupiga kazi kwa moyo bila kuchoka na hata kata tamaa huku akimpongeza Macha kwa kusema ukweli.


Mchambuzi wa soka wa kituo cha runinga cha Azam TV ambaye pia ni mwandishi, Gift Macha.


Aliongeza kuwa baada ya Macha kuandika ishu hiyo alipewa zawadi ya shilingi laki tatu kutoka kwa shabiki mmoja wa Yanga kutoka mkoa wa Morogoro ikiwa ni sehemu ya pongezi.

Kwa upande wa mashabiki ambao inaonekana ni wa Simba baada ya Macha kuweka andiko hilo walimponda Nugaz na mwandishi huyo na kumfagilia Ofisa Habari wao wa Simba, huku wale wa Yanga wakipongeza andiko hilo.

Macha aliandika namna hii:-“Binafsi navutiwa sana na utendaji na uchapakazi wa ndugu @antonionugaz ..Alianza kazi katika mazingira magumu sana pale Yanga. Hakuwa akifahamu mambo mengi ya soka. Ila hakukata tamaa.


“Kwanza anajiamini sana.. Very confident.(Mwenye kujiamini). Hata kama hajui kitu atapambana mpaka akifahamu. Ni watu wachache sana wenye moyo kama wake.


“Pili, yuko smart muda wote. Yaani kwa kifupi anajua kupendeza. Pengine ndiye Afisa Habari anayevaa Smart zaidi nchini. Mwonekano wake, unaakisi ukubwa wa Brand ya Yanga.


.

“Mwisho wa yote, @antonionugaz ameichangamsha sana Yanga. Amewafanya mashabiki kurejesha hali ya kujiamini na kujaa uwanjani katika mechi za Yanga. Inafurahisha sana.


“Mwisho lakini siyo wa yote. nimefuatilia Ukurasa wake hapa Instagram. Amejitofautisha sana na wengine.. Ameipa Yanga kipaumbele kuliko kitu kingine chochote. Nugaz anatumia muda wake wote kuisifia Yanga. Hana habari na Simba.


 


“Hapotezi muda wake kuisema vibaya Simba wala Azam.  Amechagua zaidi kuisifia Yanga. Hivi ndivyo Afisa Habari anapaswa kuwa. Hatumii muda wake kutengeneza chuki kutoka timu pinzani, ila kutengeneza upendo kwa mashabiki wa Yanga kwa timu yao.


“Natumia fursa hii kumpongeza Nugaz kwa kazi nzuri. Naamini huu ni mwanzo tu, mengi mazuri yanakuja mbeleni.”

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE