10/26/2020

Azam Wachezea Kichapo Mbele Ya Mtibwa
Azam Fc baada ya kuanza vizuri kwa kushinda mechi zote saba za ligi kuu bara, leo matajiri wa jiji la Dar es salaam, wamepoteza mchezo wao ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro kwa bao 1-0.


Goli pekee la wakata miwa limefungwa na Jaffar Kibaya dakika ya 62, bao ambalo limedumu mpaka mwisho wa mchezo.


Kwa matokeo hayo  Azam anaendelea kusalia kileleni mwa msimamo na pointi 21 baada ya michezo nane, Yanga anafuatia na pointi 19 ameshuka dimbani mara saba, Biashara United nafasi ya tatu na pointi 16 akicheza mechi nane na bingwa mtetezi Simba nafasi ya nne na pointi 13 akishuka dimbani mara nane.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger