google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Baba asimulia familia yake ilivyoteketea kwa moto | UDAKU SPECIAL

Baba asimulia familia yake ilivyoteketea kwa moto

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Baba asimulia familia yake ilivyoteketea kwa moto

Familia ya watu watano iliyokuwa ikiishi maeneo ya Pugu Stesheni jijini Dar es Salaam, imeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Oktoba 14, 2020, huku uchunguzi wa awali ukionyesha kuwa chanzi cha moto huo kikitajwa kuwa ni hitilafu  ya umeme.

 

Akizungumza hii leo baba wa familia hiyo Edward Jeremiah Katemi, amesema kuwa zoezi la kuikoa familia lilikuwa gumu  kwani hata walipojaribu kulipigia simu Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilishindwa kufika kutokana na adha ya usafiri iliyokuwepo siku ya jana kutokana na mvua kubwa iliyonyesha.

"Chanzo ni shoti ya umeme iliyopelekea nyumba yangu kuungua, madhara yaliyotokea ni mke wangu kipenzi, mdogo wangu pamoja na wanangu watatu wameniacha, chanzo ni umeme ulikatika tangu asubuhi, uliporudi ukakatika tena, nahisi uliporudi tena ulikuja kwa kasi zaidi", ameeleza, Katemi

"Tulijaribu kila njia ya kuwaokoa lakini ilishindikana kwa sababu tulikuwa sisi tu wananchi, tuliwasiliana na 'Fire' lakini wakashindwa kufika, baadaye tuliweza kubomoa ukuta na tukaanza kuwatoa lakini bahati mbaya walikuwa wamezidiwa na tulipowapeleka hospitali wakawa wamefariki", amesimulia baba wa familia.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad