Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Baba Mondi Ahaha Kumtoa Jela Amber Rutty

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREBABA mzazi wa mkali wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma amesema amepanga kutafuta fedha za kumnasua jela msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama ‘Amber Rutty’, ambaye hivi karibuni ametupwa lupango sambamba na mumewe Said Bakary.


Amber Rutty, mumewe pamoja James Charles maarufu kwa jina la James Delicious, walihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela, baada ya kushindwa kulipa faini waliyopangiwa na mahakama ya kiasi cha Sh milioni 11.


Amber Rutty na wenzake walihukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kupatikana na makosa matatu ikiwamo la kufanya mapenzi kinyume na maumbile.


Hukumu hiyo ilitolewa Septemba 25, mwaka huu na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Godfrey Isaya, baada ya kujiridhisha na ushahidi wa upande wa mashtaka kuwa washtakiwa walitenda makosa hayo.


Kufuatia hali hiyo, Baba Mondi ambaye hivi karibuni amekuwa na ukaribu na Amber Rutty, amekiri kutambua mchango wa mwanadada huyo machachari na kuweka wazi kuwa, hawezi kumwacha aozee jela.


“Yule mrembo, nimepanda naye jukwaa moja katika shoo zangu, hadi wakanizushia mambo kibao, ila watu hawajui tu ukaribu wangu naye, kwa kweli nimehuzunika sana. Kwa adhabu waliyopatiwa, nitahakikisha natafuta kiasi cha kumtoa.


“Kwa sababu Rutty bado ni kijana, hata ukiwatazama wale wenzake, ni vijana ambao bado tunawahitaji kwenye jamii… wanahitaji kujenga maisha yao,” alisema.


Baba Mondi alisema mbali na yeye, wadau wengine wanaweza pia kumuunga mkono, kwani hata yeye anasaka watu wa kumuunga mkono katika azma yake hiyo.


STORI MWANDISHI WETU, RISASI

Post a Comment

0 Comments