BASATA yaufungia wimbo wa 'one time' wa Lady JaydeeBaraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wametoa maamuzi ya kuufungia wimbo wa 'one time' ya Komando Lady Jaydee kwa kosa la kuhamasisha vitu visivyokuwa na maadili na nchi ya Tanzania.

 Meneja wa msanii huyo Mx Carter amesema kuwa siku ya leo wamepokea barua rasmi ya kufungiwa kwa wimbo huo kwenye vituo vya Radio, TV na mitandaoni. 


"Tuliitwa kwa sababu kuna vitu wao kama BASATA waliona havijakaa sawa, tukaitikia wito kwa Lady Jaydee kwenda ili kuzungumza nao, na leo tukapokea barua rasmi ya kuamua kuufungia na hautoruhusiwa kupigwa kwenye vituo vya Radio TV na kwenye mitandao kama wa YouTube" ameeleza MX Carter


"Kuna mstari ambao nisingependa kuutaja ila wanasema unahamasisha vitu ambavyo sio maadili ya kitanzania, ila kwa sisi tulivyoona haukuwa unahamasisha kwa sababu ni vitu ambavyo vipo na vitu vya kawaida" ameongeza 

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE