Beki Stars Amtetea Mbwana Samatta

advertise here


BEKI wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na Klabu ya Mtibwa Sugar, Dickson Job, amesema kuwa nahodha wa Stars, Mbwana Samatta hapaswi kulaumiwa kutokana na matokeo ya kupoteza kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafi ki dhidi ya Burundi.


Akizungumza na Championi Jumatano, Job alisema: “Tumepoteza mchezo uliopita dhidi ya Burundi lakini cha kushangaza ni kwamba watu wengi wamekuwa wakimlaumu nahodha wetu, Mbwana Samatta, lakini kwa upande wangu naamini tulipoteza mchezo kutokana na makosa ya pamoja.


“Naamini benchi la ufundi likiongozwa na kocha Ndayiragije limeyaona na litahakikisha yanafanyiwa kazi kabla ya safari yetu ya kwenda Tunisia kwa ajili ya mchezo wetu wa Novemba 13 dhidi ya timu ya Taifa ya Tunisia, katika jitihada za kuhakikisha tunafuzu michuano ya AFCON 2021,” alisema Job.


Joel Thomas, Dar es Salaam

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE