Bifu la Mondi na Harmo Lawa la Moto...Kampeni Zachochea Moto

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


BIFU la mastaa wawili wakubwa wa Bongo Fleva na mabosi wa lebo za muziki Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au ‘Mondi’ na Rajab Abdul ‘Harmonize’ au ‘Harmo’, limezidi kuwa la moto mno.

 

Hilo limezidi kuthibitika Ijumaa iliyopita, wakati wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) za Dk John Pombe Magufuli, zilizofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar.

Wawili hao wakiwa na wasanii wengine kibao, walipafomu shoo za kibabe huku Harmo akiwaburudisha mashabiki wake kwa kuwamwagia pesa, kitendo ambacho Mondi alichukulia kama silaha ya kumchapia Harmo. Katika mahojiano maalum na Global TV Online, Mondi alisikika akisema kuwa, anakusanya kijiji na kufuatwa yeye wala siyo pesa.


“Nimemaliza shoo wakati Rais anaongea, nikiondoka itakuwa siyo adabu, si unaona nimekusanya kijiji? “Mashabiki wanasema wanamtaka Diamond na siyo hela, maana wasanii wengine wanarusha hela, usiwarushie watu hela na kama wanakupenda, acha wakufuate,” Mondi aliiambia Global TV.


Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wa Harmo, walitafsiri kwamba ni kijembe kilichorushwa kwa msanii wao. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmo alimjibu Mondi kwa kusema; “Hela kwa Kijapani zinaitwa (jeshi), kwa hiyo ukisikia jeshi jeshi maana yake hela! Hela!

Au tumemuelewa vibaya? Legend bana…” Baadhi ya mashabiki walianza kuzungumza yao na kusema kuwa, mpambano unazidi kuwa moto, japo Harmo ana vijembe sana.

“Mpambano mpaka sasa ni droo, ila Konde Boy (Harmo) anashambulia sana kwa vijembe,” aliandika shabiki mmoja kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mbali na Harmo na Mondi kupanda jukwaani na kutoa shoo, wasanii wengine waliokiamsha ni Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, Faustina Charles ‘Nandy’, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ na wengine kibao.

TUJIKUMBUSHE


Harmo alikuwa ni memba wa Lebo ya Wasafi Classic Baby chini ya Mondi, kabla ya kuanzisha lebo yake mwenyewe ya Konde Gang Music Worldwide mwishoni mwa mwaka jana.


STORI: HAPPYNESS MASUNGA, DAR

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad