Bobi Wine asema polisi waliiba nyaraka za uteuzi wake wa urais

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mwanasiasa na mwanamuziki wa Uganda, Robert Kyagulanyi, al maarufu Bobi Wine, ameiambia BBC kuwa nyaraka zinazohitajikakwa ajili ya uteuzi wake wa kugombea urais zimepotea katika ofisi yake baada ya uvamizi wa ofisi hiyo wa vikosi vya usalama siku ya Jumatano mchana.

Moja ya masharti ya wagombea ni kuwasilisha sahihi za wafuasi wao 100 waliojisajili kupiga kura kutoka katika walau theluthi mbili ya wilaya za Uganda.Bobi Wine anasema timu yake ilikuwa tayari imekusanya sahihi milioni sita lakini hizi sasa zimepotea.


“Serikali ya Museveni inajaribu kunizuwia kuteuliwa kama mgombea wa urais. Kuanzia kuhoji nyaraka zangu, kuhoji umri wangu- na sasa wanafanya kila juhudi kukwamisha uteuzi wangu na ninaamini kuwa ndio maana walichukua saini .”


"Hatutakata tamaa, tumekwisha ripoti mara mojakwa matawi yetukuhakikisha wanaanza kukusanya saini mara mojana tunatumaini kufikia Ijumaa tutakuwa na saini zinazohitajika ,” alisema.


Mbunge huyo alikuwa akizungumza na BBC baada ya kutoroka kutoka katika ofisi yake wakati makumi kadhaa ya askari na polisi walipowasili kufanya msako.


Pia alisema milioni 23 Waganda milioni ($6,200 ) zilichukuliwa. Anasema pesa hizi zilichangishwa kusaidia kulipia garama za uchaguzi kwa ajili ya wanachama wanaotaka kugombea ubunge.


Polisi hawakujibu wito wa BBC wa kuzungumzia madai yaBobi Wine. Awali walikana kuwa uvamizi wa ulichocjewa kisiasa.


Tume ya uchaguzi iliwapatia wagombea siku ya Ijumaa kuwa muda wa mwisho wa kuwasilisha fomu zao za uteuzi..


Msemaji wa tume anasema hawezi kuzungumzia juu ya madai ya Bobi Wine ya kutoweka kwa nyaraka lakini anasema muda wa mwisho unaweza uongezwa kwa mgombea iwapo wataifahamisha tume rasmi.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad