google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Boris Johnson asema Uingereza ijiandae kutoelewana na Umoja wa Ulaya katika makubaliano ya biashara | UDAKU SPECIAL

Boris Johnson asema Uingereza ijiandae kutoelewana na Umoja wa Ulaya katika makubaliano ya biashara

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema leo nchi hiyo lazima ijiandae kwa kutopatikana maelewano ya kibiashara na Umoja wa Ulaya labda kuwepo na mabadiliko ya kimsimamo upande wa umoja huo. 



Johnson anasema Umoja wa Ulaya unakataa kuipatia nchi yake makubaliano ya kibiashara kama yale ya Canada, makubaliano ambayo Uingereza ndiyo inayoyatafuta. "Na kwa matumaini makubwa tutajiandaa kukumbatia mbadala. Tuwe tayari kwa Januari mosi yenye mpango ulio sawa na wa Australia ambao umetokana na msingi wa biashara huria duniani. 




Tutafanikiwa pakubwa kama nchi yenye kujitegemea na inayofanya biashara huru ambapo tunadhibiti mipaka yetu, uvuvi wetu na kujiwekea sheria zetu wenyewe."Johnson alikuwa anawajibu viongozi wa Umoja wa Ulaya ambao katika mkutano wa kilele mjini Brussels walisema UIngereza inahitajika kubadili msimamo wake ili kuwe na uwezekano wa kupatikana maelewano. 




Uingereza ilikuwa imetishia kujiondoa kutoka kwenye mazungumzo hayo iwapo makubaliano ya kibiashara hayatopatikana katika mkutano huo unaoisha leo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad