google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Bweni la shule laungua | UDAKU SPECIAL

Bweni la shule laungua

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Bweni la shule ya sekondari ya Kiislam ya African iliyoko maeneo ya Kaloleni mkoani Kilimanjaro, limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Oktoba 9, 2020, na kwamba hii ni mara ya tatu kwa shule hiyo kuungua.

 

Akizungumza leo Oktoba 9, 2020, kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kilimanjaro, Inspekta Jeremiah Mkomagi, amesema kuwa walipata taarifa za moto huo majira ya saa 1:40 usiku na mpaka wanafika eneo la tukio moto ulikuwa umeshika sehemu kubwa ya bweni.


"Tulipata wito kwamba kuna moto katika shule ya sekondari ya African Muslim na tulipofika tukakuta moto ni mkubwa sana na ni jengo la bweni la ghorofa moja na moto ulikuwa umeanzia kwenye moja ya chumba ambacho kinatumika kama stoo", amesema Inspekta Jeremiah.


Aidha Inspekta Jeremiah ameongeza kuwa "Kwenye tukio hilo hakuna majeruhi wala kifo kwa sababu wanafunzi waliondolewa mapema na kupelekwa sehemu salama, vitu vilivyoungua ni nguo zao, vitanda na madaftari, chanzo hakijabainika kwa sababu kumekuwa na mlolongo wa shule kuungua na hii ni mara ya tatu".


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad