10/04/2020

CHADEMA wakiri Tundu Lissu kutofanya kampeni

 


Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyokaa jana imemshauri mgombea wao wa urais Tundu Lissu kutofanya kampeni katika kipindi hiki akitumikia adhabu ya kufungiwa siku saba na Kamati ya Maadili ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

 

Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Slaam Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe amesema kwamba hata hivyo wanaipinga adhabu hiyo na watafungua kesi kwa hati ya dharura Mahakama Kuu kupinga maamuzi hayo.


Kamati Kuu ya Chadema pia imeridhia kumuunga mkono mgombea urais Zanzibar Seif Sharif Hamad kupitia chama cha ACT-Wazalendo, na wameanza mchakato wa kujitoa kwa mgombea urais wao wa Zanzibar.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger