Chama Cha Mapinduzi Babati Mjini kimeshinda Kata zote

Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Babati Mjini kimepita kwa kishindo katika nafasi ya Udiwani  kwenye  kata zote nane za Jimbo hilo lililopo mkoani Manyara.


Kabla ya Uchaguzi mkuu kufanyika Kata za Nangara na Babati Mji zilikuwa zinashikiliwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi Jimboni hapo Fortunatus Fwema amesema Madiwani hao wanasubiri kupatiwa Vyeti vya kutambuliwa na baadaye kuapishwa rasmi.


Pamoja na hayo, Msimamizi huyo amemkabidhi cheti  cha utambuzi Mbunge Paulina Gekul (CCM) aliepita bila kupingwa.


Jimbo la Babati Mjini lina kata nane ambao ni Maisaka, Mutuka, Sigino,Bonga,Nangara, Singe, Bagara na Babati Mji.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE