DC Sabaya - Askari nao ni binadamu wanachukia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, amesema hakuna Askari aliyemzuia Mbowe kufanya kampeni na kwamba hata video inayosambaa mitandaoni ikimuonesha yeye na Askari wakibishana ni kwa sababu alivunja utaratibu kwa kutaka kufanya kampeni eneo ambalo hakutakiwa kinyume na kanuni za Tume.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Oktoba 10, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, alipoulizwa alichukuliaje kitendo cha Askari kumzuia mgombea kufanya kampeni huku akidai mgombea huyo hawezi kumshinda mgombea wa chama fulani, ambapo amesema kuwa Askari huyo alifika pale kwa lengo la kuwaweka sawa kwani eneo hilo kulikuwa na mgombea mwingine.




"OCD alifika pale kuhakikisha makundi mawili hayahitilifiani na Mbowe alifanya makusudi na aliambiwa aondoke ndiyo mabishano yakatokea, Jeshi la polisi ni chombo cha dola na wanaolitumikia ni binadamu nao wanafika mahali wanakasirika, kwamba kila mahali ni kuwanyoshea kidole kama alivyozoea ni bora angeendelea kunitukana mimi lakini siyo yule mtu mzima watu wasione matukio ya mwisho ya mtu aliyedhihakiwa halafu wang'ang'anie huyu mwingine", amesema DC Sabaya




"Aliyevunja taratibu ni huyu mgombea ubunge, naamini Tume nayo itachukua hatua hamuwezi kuweka sheria wenyewe na mnazivunja, halafu mnatafuta huruma nyepesi kwa sababu mmeshindwa kuomba kura, unageuza agenda ya kuomba kura ili ujipatie huruma hiyo haikubaliki kabisa", ameongeza DC Sabaya.




Oktoba 7 mwaka huu ilionekana video mitandaoni ikimuonesha Askari Polisi wilayani Hai, akibishana na mgombea ubunge wa jimbo hilo Freeman Mbowe kuhusu ufanyaji wa kampeni huku Askari huyo akidai kuwa Mbowe hawezi kumshinda mgombea wa chama kingine ambaye hakumtaja jina.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad