10/12/2020

Hamilton aifikia rekodi ya Michael SchumacherDereva wa magari kutoka timu ya Mercedes Lewis Hamilton, ameshinda mbio za Formula 1 Eifel GP huko Nurburgring Ujerumani

Hamilton alionekana kuwa vizuri tangu mwanzo wa mbio ambapo mara chache wenzake walifanikiwa kumzidi lakini mara nyingi aliongoza mbio.

Baada ya ushindi huo muingereza huyo saa ameifikia rekodi ya nguli Michael Schumacher ya kushinda mara 91 katika mbio hizo za Eifel GP.

Baada ya kushinda Hamilton alikabidhiwa kofia ngumu (helmet) na mtoto wa Schumacher aitwaye Mick Schumacher kama ishara ya heshima.

Mick Schumacher kwasasa ni dereva wa Formula2 kupitia academy ya timu ya Ferrari na anaongoza msimamo wa Formula2 msimu huu.

Nafasi ya pili kwenye mbio za leo, imeshikwa na Max Verstappen wa Red Bull na nafasi ya nne imeenda kwa Daniel Ricciardo wa Renault.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger