10/26/2020

Dkt. Magufuli: Tulijenga Msikiti leo utafunguliwa na Mufti wa Tanzania na Mimi nataka niwahi pale ili tupate Baraka za Mungu


Mgombea Urais wa Tanzania kwa Ticket ya CCM, Dkt.John Pombe Magufuli tayari ameingia Dodoma akitokea Manyara kwenye mwendelezo wa kampeni, akiwa Chamwino leo amewaomba kura Wananchi na kuwaombea kura Wabunge na Madiwani na kisha kuwaaga akisema ana ratiba nyingine ya ufunguzi wa Msikiti.

“Nawashukuru sana nina ratiba nyingine nataka niwahi Chamwino tulijenga Msikiti leo utafunguliwa na Mufti wa Tanzania na Mimi nataka niwahi pale ili tupate Baraka za Mungu kwa siku ya leo, nawaomba msidanganywe na fujo, tuitunze amani yetu, penye amani pana maendeleo” -JPM


Itakumbukwa Jumapili ya August 23,2020 JPM alihudhuria Misa Takatifu na uzinduzi wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Imakulata,Ikulu Chamwino, Dodoma, ambapo alisema Waislamu pia walichangia ujenzi wa Kanisa hilo na kuwataka na Wakristo kuungana na Waislamu kuchangia ujenzi wa Msikiti Chamwino kupitia harambee aliyoiendesha Kanisani hapo.


JPM alisema "Kwenye michango tuliyochangisha hapa Kanisani, tumepata jumla ya Tsh.Milioni 48 na Eflu 21, mifuko 48 ya cement na Lori 5 za mchanga, Rostam amechangia Mil 20, Boss wa CRDB Nsekela Mil 10, pia CAG Kachere, Anthony Mavunde, RC Dodoma ni miongoni mwa waliochangia, sasa Msikiti utajengwa, Mimi nina Wasaidizi wangu wengine Waislamu yupo hadi El Hadji, wataswali kwenye Msikiti huo"

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger