10/09/2020

EXCLUSIVE: Mondi Afunguka Kashfa Kutumiwa na CCMMSANII wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, amefunguka ukweli kuhusu wasanii wengi kutimkia kwenye kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinazoendelea nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 huku vyama vya upinzani vikikosa wasanii katika kampeni zake.


 


Mondi amefunguka hayo leo mara baada ya kufanya shoo kwenye kampeni za mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. John  Magufuli zilizofanyika katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

“Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuturahisishia, amefanya kazi kubwa na sisi sote tumeiona, ndiyo maana hata kampeni zimekuwa rahisi, zamani tulikuwa tukifanya kampeni tunatukanwa, sasa hivi hakuna, hivyo tunamuunga mkono, bega kwa bega, chocho kwa chocho.

“Nimetoka tu nje hapa kijiji kinataka niamshe, nasubiri Mheshimiwa Rais amalize kuzungumza, wasanii wengine wanakosea huwezi kuwarushia mashabiki pesa ili wakufuate, kama wanakupenda acha watu wakufuate.

“Nimeanza kumsapoti Magufuli tangu anaingia, nimekuwa CCM tangu zamani kwa hiyo wanaosema wasanii hatujaenda upinzani hayo ni ya kwao. Magufuli ameleta maendeleo sana kwenye nchi yetu, maendeleo niliyoyapata mimi ni kwa sababu ya mambo aliyofanya JPM.


“Nimeenda nchi nyingi sana hususani za Afrika, kila mmoja anatamani uongozi wa Dkt. Magufuli, Cameroon kuna mpaka msanii amemuimba Magufuli, hii inaonyesha rais wetu anavyopendwa,” amesema Diamond.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger