Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Faiza Amtuliza Sugu Baada ya Kushindwa UbungeMFANYABIASHARA Faiza Ally amempa moyo na kumuunga mkono aliyekuwa mpenzi wake wa zamani na baba mtoto wake, Joseph Mbilinyi ‘Mr II Sugu’, baada ya kushindwa nafasi ya Ubunge kwenye Jimbo la Mbeya Mjini ambaLo limekwenda kwa Dkt Tulia Ackson wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


 


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Faiza ameandika maneno ya kumtia nguvu mzazi mwenzake huyo kufuatia kushindwa kutetea nafasi yake ya Ubunge wa Jimbo hilo kwa kura 37,561 dhidi ya kura 75,225 ambazo amezipata Dkt Tulia Ackson.


 


“Tulikupendaga, tuliendelea kukupenda, tunakupenda zaidi na tutakupenda kila siku, machoni mwetu na kwenye mioyo yetu wewe ni mshindi toka mtoto mpaka utazeeka na mpaka siku ya mwisho itakuwa hivyo hakuna kitakachobadilika, mimi na familia tunakutumia salamu za upendo tunatamani kuwepo ulipo tusheherekee maisha pamoja kwa sababu wewe ni mshindi kwetu, najivunia wewe baba Sasha,” ameandika Faiza Ally.


 


Joseph Mbilinyi anawakilisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), aliongoza Jimbo la Mbeya Mjini kuanzia mwaka 2010 hadi 2020, ambapo kuanzia sasa litaongozwa na Dkt. Tulia Ackson kama ambavyo msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Mbeya Mjini alivyomtangaza kushinda nafasi ya ubunge wa imbo hilo

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments