10/11/2020

Fraga, Bocco Chini ya Uangalizi SimbaMASTAA wa Simba, jana wameanza mazoezi ya gym huku kiungo wa timu hiyo Gerson Fraga na mshambuliaji John Bocco wakiwekwa chini ya uangalizi maalum wa daktari.


Fraga aliumia nyonga katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Biashara na kusababisha atolewe dakika ya sita huku Bocco ambaye aliitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars akiondolewa na Kocha Etienne Ndayiragije kwa madai kuwa alikuwa na majeraha aliyotokanayo Simba.


Simba chini ya Kocha Mbelgiji, Sven Vandenbroeck walikuwa kwenye mapumziko tangu walipomaliza mchezo wao wa Jumapili iliyopita dhidi ya JKT Tanzania ambapo Msimbazi walishinda mabao 4-0.

Akizungumza na Championi Jumamosi, meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu alisema kuwa tayari wamerejea kambini kuendelea na maandalizi ya mechi zao zijazo baada ya mapumziko ya siku tatu.

“Tumeingia kambini leo (jana) kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mechi zetu za mbele baada ya mapumziko mafupi ya siku tatu tangu tumerejea Dar katika mchezo wetu na JKT Tanzania kule Dodoma.

“Kwa upande wa mazoezi, tumeanzia Gym kwa wachezaji wote ambao hawajasafi ri kwenda kwenye timu zao za taifa kwa ajili ya mechi za kimataifa lakini wachezaji wetu John Bocco na Gerson Fraga bado wapo kwenye uangalizi maalum wa daktari kutokana na majeraha wanayouguza,” alisema Rweyemamu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger