Haji Manara Aibuka Tena...Aipongeza AZAM FC Kwa Kukaza...Adai Simba Itachukua Ubingwa, Yanga Itashika Nafasi ya Tatu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Baada ya Klabu ya Azam FC kuwa na muendelezo mzuri kwenye Ligi Kuu soka Tanzania Bara msimu huu, msemaji wa Simba @hajismanara amesema wanaweza kushika nafasi ya pili nyuma yao huku akiwatabiria watani zao Yanga kumaliza katika nafasi ya tatu msimu huu.


Azam FC jana wamepata ushindi wao wa bao 3-0 dhidi ya Mwadui ya Shinyanga hali iliyopelekea Haji Manara kuandika kupitia ukurasa wake wa Instagram juu ya ubora wa kikosi cha wanalamba lamba hao.


Manara ameandika, “Kwa mwenendo huu naiona Azam Fc ikipigania taji msimu huu, mna kikosi kizuri na kwakweli mnastahili hongera.Timu inayopigania mataji huwa hailalamiki lalamiki hovyo, huwaoni na makabrasha TFF wala FIFA au CAS.”


“Hamkupokea mchezaji kwa mbwembwe bandarini wala stendi ya Ubungo lakini manonesha mlivyodhamiria. Najua msimu huu mtakamata nafasi ya pili nyuma ya championi wa Taifa hili, yule wa tatu mtamuacha kwa pointi ishirini na tano” Haji Manara.


Ushindi wa Azam umewafanya wafikishe alama 18 katika mechi 6 walizocheza msimu huu.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad