IGP Sirro aagiza uchunguzi polisi aliyemwambia Mgombea Ubunge Freeman Mbowe hatashinda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro, amesema timu kutoka Makao Makuu ya jeshi hilo iko mkoani Kilimanjaro kufanya uchunguzi wa video ya ofisa wa polisi anayedaiwa kumwambia Mgombea Ubunge wa Hai (CHADEMA), Freeman Mbowe, hatashinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.


Video hiyo iliyosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii katikati ya wiki hii, inamwonyesha ofisa huyo wa polisi akijibizana na Mbowe, ofisa huyo akisikika akisema 'utamshinda yule? huwezi kumshinda, unawadanganya wananchi kuwa utamshinda."


Katika majibizano hayo, ofisa huyo aliyekuwa na mavazi ya Jeshi la Polisi, pia alisikika akimwambia Mbowe kuwa anasababisha watu wanamfuata na kumtaka aingie kwenye gari.


“Mnafanya watu wanakuja, ingia kwenye gari tuondoke," alisikika ofisa huyo huku Mbowe akimjibu "sawa, msinifukuzie watu wangu, watu wanifuate niwakimbie, hapana!”


Baada ya Mbowe kutoa kauli hiyo, ofisa huyo akasema: “Huwezi kumshinda hata ufanyaje, humshindi, ingia kwenye gari uondoke, yaani mawazo yako unawadanganya wananchi utamshinda, humshindi."


Akizungumza kuhusu video hiyo jana, IGP Sirro alikiri kuiona na kuweka wazi kwamba, tayari timu kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi imekwenda kulichunguza tukio hilo kwa kuwa kabla ya kufanya uchunguzi, hawapaswi kulaumu pande zote mbili.


“Nimeiona video hii na tunavyozungumza, timu yetu kutoka Makao Makuu tayari imekwenda kuchunguza hilo tukio kuona kuna nini. Suala la majibu kwamba utashinda au utashindwa, hiyo siyo kazi ya polisi, ni kazi ya tume (Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC).


"Tunachunguza, tukiona kuna jambo la ukweli kutokana na ile video tuliyoiona, basi tutachukua hatua dhidi ya huyo ofisa. Jeshi lina kanuni zake na tuna kanuni za kudumu, wanasema 'Police General Order', ile inatuongoza sana, lakini pia tuna sheria za Jeshi la Polisi na za maofisa wasaidizi pia na maelekezo." alisisitiza.

 

Msikilize hapo chini 



"Tunachunguza tukio la video iliyosambaa mtandaoni na timu yetu kutoka Makao Makuu ipo Hai mkoani Kilimanjaro ikiendelea na uchunguzi" IGP Sirro#UmojaWetuNdioNguvuYetu pic.twitter.com/Ze0MReVZ98


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. IGP, alicho kisema Afande kwa Faru Joni ni ukweli mtupu
    kwa Afande amemkumbusha baada ya kutokea Janga la Corona huyu alihamasisha wenzake kusepa Uwakilishi Bungenni

    ReplyDelete
  2. IGP, alicho kisema Afande kwa Faru Joni ni ukweli mtupu
    kwa Afande amemkumbusha baada ya kutokea Janga la Corona huyu alihamasisha wenzake kusepa Uwakilishi wa hawa wananchi
    waliomtuma Bungeni, sasa afande baada ya kujumlisha ukweli huu.. Kwa NIA njema kabisa amemtanabahisha huyu mgombea ili
    iwe ni kumbusho kwake kuwa wananchi sio wajinga wanaona na
    kusikia. kama ni zezeta wa ni wewe uko katika wakati mgumu
    katka kipindi hiki chautekelezaji ulliotukuka wa JPM.

    Hata ingeuwa mimi, Ningemwambia usijipotezee wakati tafuta
    ukumbi mwinginee uendelee kupiga disco. Siasa huiiwezi.

    ReplyDelete

Top Post Ad