Kafara ya Harmo Yaanza KujibuKufuatia ripoti zilizoanza kutoka wiki iliyopita za mafanikio ya wasanii kumtaja staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’, kuwa miongoni mwa mastaa wanaovuma zaidi na kuwa na mafanikio makubwa nchini Tanzania na Afrika Mashariki, watu wametia neno huku ile kafara aliyofanyiwa mapema mwaka huu, ikitajwa kujibu.

UTAJIRI WA BIL. 2


Mitandao mbalimbali inayodili na kukusanya data za ukwasi wa wasanii Afrika Mashariki, yote imemtaja Harmonize au Harmo kufanya vizuri kimuziki kwa mwaka 2020 na kutia kibindoni Dola za Kimarekani bilioni moja (zaidi ya shilingi bilioni 2 za Kitanzania).


Baada ya kujitoa kwenye Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) chini ya msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, miezi kadhaa iliyopita, Harmo alifanyiwa kafara la damu la kutisha huko nyumbani kwao mkoani Mtwara.


Kafara hiyo iliambatana mbuzi kuchinjwa na wazee, kisha Harmo alinyweshwa damu yake mbichi na nyingine alipakwa usoni, kifuani na miguuni huku akinenewa maneno ya kilugha.


LENGO KUMFUNGULIA MILANGO


Kwa mujibu wa wazee wake waliomfanyia kafara hiyo ya damu, lengo lilikuwa pamoja na kumewekea ulinzi, lakini pia kumfungulia Harmo milango ya mafanikio.


KAFARA IMEJIBU?


Sasa basi, miezi tisa baada ya tambiko hilo, baadhi ya watu wake wa karibu wanajimwambafai kuwa, kafara hiyo imeanza kujibu na kumfanya jamaa huyo kuwa na mafanikio makubwa kwenye muziki wake.


Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, 2019 ulikuwa mwaka wa mapinduzi kwa Harmo baada ya kuamua kuikacha WCB na kuanzisha lebo yake ya muziki ya Konde Gang Music Worldwide.


NDANI YA MWAKA MMOJA


Imeelezwa kwamba, katika kipindi cha mwaka mmoja tu, Harmo amejipanga vya kutosha na kutengeneza mtandao wa kuweza kumuunga mkono. Inasemekana kwamba, hilo limejidhihirisha kwani ameendelea kufanya vizuri kwa kutoa nyimbo kali na zilizobamba na kumuongezea mamilioni ya mashabiki.


ALBAM YA AFRO EAST


Zaidi, katika kipindi hicho, inaelezwa ndipo alipofanikiwa kuachia albam yake ya Afro East, jambo ambalo hakuweza kulifanya akiwa ndani ya WCB.


Ni katika albam hiyo yenye jumla ya nyimbo 17, ambapo amefanikiwa kushirikiana na wasanii wakubwa na maarufu wa ndani na nje ya Bara la Afrika akiwemo Yemi Alade (Nigeria), Lady Jaydee na Nandy (Tanzania), Morgan Heritage (Jamaica), Skales (Nigeria), Khaligraph Jones (Kenya) na wengineo.


WASANII WAKE


Pia vyanzo hivyo vimempa tano Harmo, kwani sambamba na kujisimamia binafsi, tayari lebo yake hiyo imesaini wasanii kama Ibraah, Cheed, Killy, Country Wizzy na kumsimamia Slakes wa Nigeria kwa upande wa Afrika Mashariki.


ALBAM YA PILI


Katika mahojiano na gazeti hili hivi karibuni, Harmo aliweka wazi kuwa, yupo mbioni kuachia albam nyingine ya pili kabla mwaka huu haujageuka. “Ni kweli natamani kuachia albam nyingine mwezi Novemba, mwaka huu,” alisema Harmo.


UTAJIRI SASA


Kwa mujibu wa mitandao hiyo, mbali na ukwasi huo wa zaidi ya bilioni 2 huku akimfukuzia aliyekuwa bosi wake, Diamond au Mondi anayetajwa kuwa na utajiri wa zaidi ya shilingi bilioni 11, pia Harmo anaishi maisha bomba kwenye mjengo wa kifahari uliopo ufukweni mwa Bahari ya Hindi, maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar wanapoishi washua.


STUDIO KALI

Harmo anamiliki studio kali ya kurekodi muziki ya Konde, ambayo ipo kwenye mjengo wa kifahari yalipo makao makuu ya lebo yake hiyo maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar.


MAGARI YA KIFAHARI


Mbali na yeye mwenyewe kusukuma magari ya kifahari kama Toyota Land Cruiser V8, Audi, Toyota Alphard na mengineyo, pia amewapa magari wasanii wake wawili, Country Wizzy na Ibraah, lakini kabla ya hapo, alimpa pia msanii Q-Chillah.


WAZAZI


Ukiacha wasanii wenzake, Harmo pia amewanunulia wazazi wake magari aina ya Toyota Harrier kila mmoja na kuwajengea nyumba ya kifahari kijijini kwao, Chitoholi mkoani Mtwara.


HARMO ANASEMAJE?


Katika mahojiano mbalimbali juu ya mafanikio yake, Harmo amekuwa akisisitiza; “Nikitazama nilipotoka kijijini kwetu Mtwara, namshukuru sana Mungu kwa kunijaalia maisha niliyonayo. “Pili sitaacha kumshukuru sana Diamond maana amechangia mimi kuwa hapa nilipo leo.”


Stori Sifael Paul, Risasi Stori Mashauri Samwel na Samson Johnson

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE