Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kagere Atoa Kauli ya Matumaini SimbaSTRAIKA wa Simba, Meddie Kagere ametoa kauli ya matumaini kwa kusema yupo kwenye muda wa kurikava majeraha yake ambapo baada ya muda atarejea katika majukumu yake.


 


Kagere ameongeza kwamba kwa kipindi hiki anapumzika kwa ajili ya kujiweka salama baada ya kupata majeraha kwenye mechi iliyopita mbele ya JKT Tanzania.


 


Straika huyo ameachwa Dar kwenye msafara wa kikosi cha Simba ambacho kilienda Sumbawanga na kesho Alhamisi kitacheza dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Nelson Mandela.
Nyota huyo mwenye mabao manne amesema kwamba kwa kipindi hiki anaendelea kupata muda wa kupumzika akiuguza majeraha yake ambapo baada ya muda atarudi katika majukumu yake.


 


“Kwa sasa niko kwenye wakati wa kurikava baada ya kuumia, nimepewa siku za kupumzika naamini nitarudi katika mazoezi ya kawaida siku chache baada ya sasa,” alimaliza Kagere.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments