10/18/2020

Kagere Azua Hofu Simba, Kuwakosa YangaHII inaweza kuwa habari mbaya sana kwa Simba baada ya straika wao Mnyarwanda, Meddie Kagere kuwa hatarini kuikosa mechi ya watani wa jadi dhidi ya Yanga kutokana na majeraha.


Taarifa hizo zimezua hofu kwa Wanasimba na huenda straika huyo akaikosa mechi hiyo iliyopangwa kuchezwa Novemba 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. Awali mechi hiyo ilipangwa kuchezwa leo Jumapili, lakini Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ikaisogeza mbele.


Majeraha ambayo yanamsumbua Kagere, yatamfanya kukaa nje ya dimba kwa takribani wiki tatu ili apone kabisa, kisha kuanza mazoezi ya kuwa fiti kurudi uwanjani.

Uongozi wa Simba kupitia kwa Ofisa Habari, Haji Manara, amesema straika huyo ameongezeka kwenye listi ya majeruhi kikosini kwao ambapo atakuwa nje kwa wiki tatu chini ya uangalizi maalum.

Wachezaji wengine wa Simba ambao wana majeraha ni Gerson Fraga na John Bocco


“Tunao wachezaji majeruhi, Gerson Fraga ambaye anaendelea vizuri, John Bocco ameshaanza mazoezi mepesi. Mwingine ni Meddie Kagere ambaye kwa mujibu wa jopo la madaktari atakaa nje kwa takribani wiki tatu mpaka pale hali yake itakapotengemaa, atarejea uwanjani.


“Matarajio yetu Wanasimba wataendelea kuwaombea wachezaji wetu ambao wamepata majeraha kwa ajili ya kuitumikia timu hii,” alimaliza Manara.


Kutokana na kauli hiyo, wiki tatu kuanzia kutoka kwa taarifa hiyo juzi Ijumaa, ni sawa na siku 21 ambapo Kagere atapona Novemba 6, hivyo hadi kuwa fiti kabisa, itamfanya kusubiri zaidi na kuikosa mechi hiyo ya Novemba 7.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger