Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kanye, Malone Wang’ara Tuzo za BillboardMSANII Post Malone na rapa  wa  miondoko ya Hip Hop kutoka Marekani aliyegeukia muziki wa Injili, Kanye West, wamen’gara kwenye tuzo  Billboard Music Award, baada ya Malone kushinda tuzo nane kati ya 16 na Kanye kushinda tuzo nne kati ya nane alizokuwa anagombania.


 


Sherehe za utoaji wa tuzo hizo zilifanyika jana Alhamisi  kwenye ukumbi  wa Dolby Theatre, Los Angeles .


 


Kanye ameshinda tuzo nne za Billboard zikiwemo Top Gospel Artist, Top Christian Album, Top Gospel Album (Jesus Is King) na Top Gospel Song (“Follow God”).


 


Msanii huyo ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki (Producer) alikuwa akishindania tuzo nane na amefanikiwa kupata nne.  Pamoja na kutoweza kuhudhuria tuzo hizo,  alipata nafasi ya kuwashukuru waandaji wa tuzo hizo akisema amefarijika sana kushinda tuzo hizo kubwa nchini marekani na hiyo imeonyesha kwa jinsi gani mashabiki wake wanavyoendelea kumuunga mkono hata baada ya kuhamia kwenye muziki wa Injili.
 


Mke wa rapa huyo, Kim  Kardashian,  pia alitumia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram kumpongeza baba watoto wake na kuzima tetesi kuwa wawili hao walikuwa hawaishi pamoja baada miezi michache iliyopita kudai talaka kwa madai kuwa Kanye alimdhalilisha.


 


Tuzo hizi   zilizopaswa kufanyika mwezi Aprili  ziliahirishwa kutokana na janga la Corona. Wasanii mbalimbali waliimba bila kuwa na mashabiki ndani ya ukumbi, wengi wao wakifuatilia tuzo hizi kupitia runinga.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments