Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kauli ya Simba Baada ya Mchezo wao na Yanga Kusogezwa Mbele

 


 UONGOZI wa Simba umesema kuwa umepokea taarifa za kupelekwa mbele kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga uliopangwa kuchezwa Oktoba 11 kutoka kwa Bodi ya Ligi Tanzania.

Leo Oktoba 7 ilikuwa zimebaki siku 11 kabla ya beto hiyo kupigwa Oktoba 11 ila kwa sasa itakuwa mpaka Novemba 7, Uwanja wa Mkapa.


Mkurugenzi wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa wamepokea taarifa hizo za kupelekwa mbele mchezo huo hivyo wanazifanyia kazi.


"Tumepokea taarifa kupelekwa mbele kwa mchezo wetu na tutazifanyia kazi kwa ukaribu ndani ya Simba," amesema.


Kabla ya dabi hiyo timu zote mbili zilikuwa zimecheza jumla ya mechi tano ambapo zote zina pointi 13 kibindoni.


Simba yenyewe ipo nafasi ya pili na Yanga nafasi ya tatu kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments