Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Kaze: Huyu Faridi, Nyie Acheni

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREKOCHA Mkuu wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze amemwagia sifa kiungo wake mshambuliaji Farid Mussa huku akimuhakikisha nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.


 


Hiyo ni baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi wakati timu hiyo ilipocheza na Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa juzi Alhamisi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.


 


Nyota huyo awali hakuwa na nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu kilichokuwa kinafundishwa na Kocha Mserbia Zlatko Krmpotic aliyesitishiwa mkataba wake.


 


Akizungumza na Championi Jumamosi, Kaze alisema kuwa amemtazama kiungo huyo mara nne katika mazoezi ya timu hiyo kambini kwao Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya Dar na kugundua kitu kwake.


Kaze alisema kuwa kiungo huyo ana uwezo mkubwa wa kufunga, kutengeneza mabao huku akitumia mguu wake wa kushoto kukokota mpira wakati wa kushambulia goli la wapinzani.
Aliongeza kuwa, anavutiwa zaidi na aina yake ya uchezaji wa kasi akiwa na mpira akiwafuata mabeki wa timu pinzani na kuwapiga chenga, kitu hicho alikifanya katika mchezo huo na kuzaa bao la Mkongomani, Mukoko Tonombe ambaye alipokea pasi ya Farid.


 


“Farid ni aina ya wachezaji ninaotaka wawepo katika kikosi changu cha kwanza na hiyo ni kutokana kuijua falsafa yangu ambayo ni kucheza soka la pasi na kasi wakati timu ikiwa na mpira.


 


“Ni mjanja akiwa na mpira na haogopi mabeki wa timu pinzani ambaye yeye akiamua kulazimisha mashambulizi kwenye goli la wapinzani anaweza, kama ulikuwa unamfuatilia vizuri (leo) juzi utagundua kitu kwake.


 


“Hivyo nimepanga kuendelea kumtumia katika michezo ijayo ya ligi na mashindano mengine katika kuhakikisha timu yangu inapata matokeo huku nikiendelea kutengeneza timu taratibu,” alisema Kaze.

Post a Comment

0 Comments