10/06/2020

Kiba, Mondi Waoneshana UmwambaWakali wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Salehe Kiba ‘Kiba’ ambao wamekuwa wakiwagawa mashabiki kama zilivyo timu za Simba na Yanga, kila mmoja amendelea kuonesha umwamba katika shoo wanazopiga kwenye kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM).


 


Hali hiyo imechochea ubishi kwa mashabiki wao baada ya wasanii kupanda jukwaa moja katika kampeni hizo ambazo CCM imebeba wasanii lukuki wanaochagiza mwamko kwa wananchi kusikiliza sera za chama hicho.


 


Juni 12, mwaka huu, Rais Dk John Magufuli ambaye pia Mwenyekiti wa CCM aliwakutanisha wasanii hao kwa mara ya kwanza alipowaalika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, mualiko alioutoa kwa wageni wote walioalikwa kwenye mkutano mkuu wa CCM Dodoma.


 


Aidha, Agosti 29 wasanii hao ambao ni mahasimu wakubwa katika gemu ya muziki wa Bongo walikutanishwa tena katika jukwaa la kampeni za chama hicho ambacho kilizindua rasmi kampeni zake huko jijini Dodoma.


 


UMWAMBA WATAWALA


Aidha, katika mwendelezo wa kampeni za chama hicho ambazo zinajaza nyomi ya wananchi na makada kindakindaki wa CCM, wasanii hao wameendelea kuonesha umwamba kwa kutumia ubunifu wa aina yake katika shoo hizo.
MONDI


Mondi ambaye sasa anatafsiriwa kuwa Staa namba moja Bongo na Afrika Mashariki, ndiye anayezidi kukonga nyoyo za mashabiki wake kwa kile kinachelezwa kuwa anaweza kuliteka jukwaa.


 


Mondi ambaye anatamba na ngoma ya Linawachoma aliyoshirikana na Zuhura Othman ‘Zuchu’, anasifika kwa kuwa na ubunifu wa kipekee awapo jukwaa pindi anapopanda na madansa wake ambao nao hupikwa na kupikika.


 


Hilo limethibitika katika kampeni za CCM mikoa ya Mbeya na Songwe ambako Mondi aliangusha shoo ya kibabe na kuwapa raha ya kipekee wananchi ambao walilazimika kumfuata hata baada ya kumaliza shoo na kusepa.


 


Mmoja wa mashabiki waliotinga uwanjani hapo, Evance Mwakatwila alisema Mondi amedhihirisha kuwa baba lao kwa shoo kali aliyoiangusha kwenye mkutano huo wa Mbeya.
KIBA


Licha ya Mondi kupangwa kuwa msanii wa mwisho kutumbuiza katika majukwaa hayo ya kampeni, Kiba anapopanda jukwaa huwaburudisha mashabiki kutokana na sauti yake kusheheni vionjo vya ala za muziki jambo ambalo linaelezwa kumbeba kijana huyo wa Kigoma mwenye kipaji cha kipekee.


 


Licha ya Kiba kutokuwa na ubunifu mkubwa wa kuchangamsha hadhira kama ilivyo kwa Mondi, mkongwe huyo wa Bongo Fleva amethibitisha heshima yake kutokana na muziki wake kukubalika kwa mashabiki nchini.


 


Hali hiyo inadhihirishwa na wananchi wanaohudhuria kampeni hizo ambapo huimba pamoja naye huku akishibihisha kwa sauti yake yenye vionjo vya kipekee.


 


Aidha, wananchi hao waliojitambulisha kwa majina ya Geroge Mwamaja na Malela Mwakatobe kutoka Igawilo, walisema moja ya sababu ya Kiba kuendelea kumfunika Mondi ni uwezo wake wa kuimba kwa ubora huku akibebwa na sauti yake ambayo huwachoma mashabiki na kulazimika kufurahia vionjo vyake.


 


WAKABANA KOO YOUTUBE


Wakali hao wa burudani wameendelea kutunishia misuli hata katika ngoma zao walizotoa hivi karibu ambapo wakati Kiba anatamba na kibao cha cha Mediocre, Mondi kwa kushirikiana na Zuchu naye alifyatua Litawachoma, ngoma ambazo zote zimejaa vijembe na tambo za aina yake.


 


Ngoma hizo hadi kufikia Oktoba Mosi zilikuwa zimefungana kwenye mtandao wa Youtube kwa kutazamwa mara milioni 1.7 kila mmoja lakini wimbo wa Kiba ukiwa umetoka siku sita kabla ya kufikia Oktoba Mosi wakati ule wa Mondi ukiwa umetoka siku tatu kabla.


 


Mastaa hao wenye mashabiki wengi nchini, kila mmoja anatamba kwa kuwa mfalme huku wakijinasibu kwa kujipa majina ‘a.k.a’, kama vile Simba kwa upande wa Diamond ilihali Kiba ‘King’ akijiita Mfalme.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger