Killy Akiri Bado Kumkumbuka Ali Kiba na Kings Music Kwa Ujumla...

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Msanii wa Konde Gang @officialkilly_tz ameikumbuka lebo yake ya zamani Kings Music Records kwa kusema hajafuta na hawezi kufuta namba za wasanii aliowaacha kwenye lebo hiyo kwani bado ni familia yake ila kilichobadilika ni kuhamia upande mwingine katika harakati za kimuziki.


Killy amesema hivyo mbele ya waandishi wa habari baada ya kujibu tetesi ambazo zinadai kuwa amefuta namba za wasanii wa Kings Music Records na hawana mawasiliano tena baada ya kusainiwa Konde Gang ya Harmonize.


“Hizi ni harakati na maamuzi pia ni muendelezo wa maisha ya muziki, Konde Gang wamenipokea kwa mikoni miwili, kuna upendo sana na tunaishi kifamilia kabla ya kazi, sijafuta namba ya mtu yeyote kila kitu kipo vilevile wale bado ni ndugu zangu na hatujagombana sijaongea na Alikiba ila Abdukiba nazungumza naye” amesema Killy 


Killy na Cheed walitangaza kujitoa Kings Music Records ya Alikiba siku ya Aprili 14, 2020 ambapo kwa sasa wapo lebo ya Konde Gang chini ya msanii Harmonize.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad