Kisa Simba…GSM Yawaita Mastaa Saba…

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



BAADA ya Yanga kufanikiwa kumuongezea mkataba wa miaka miwili beki wao Mghana, Lamine Moro, wadhamini wa timu hiyo ambao ni Kampuni ya GSM, wamepanga kuiboresha mikataba ya wachezaji wao wote ambao inaelekea ukingoni kumalizika.


Matajiri hao wa GSM, juzi walifanikisha kumuongezea mkataba Lamine ambao unamfanya kuendelea kuwa ndani ya kikosi cha Yanga hadi 2023.

Hivi sasa kuna mastaa saba wa Yanga ambao mikataba yao ipo mbioni kumalizika ambao ni Haruna Niyonzima, Mapinduzi Balama, Said Juma Makapu, Farouk Shikalo, Metacha Mnata, Abdulaziz Makame na Deus Kaseke.GSM imepanga kuwaongezea fasta mastaa hao ili kuwazuia Simba wasiwachukue kama ilivyokuwa kwa Bernard Morrison raia wa Ghana ambaye aliichezea Yanga kwa takribani miezi sita, kisha akajiunga na Simba baada ya mkataba wake kumalizika.

Akizungumza jijini Dar, Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM na Makamu Mwenyekiti wa Usajili wa Yanga, Injinia Hersi Said, alisema kuwa zoezi hilo la kuwaongezea mikataba wachezaji wao wamepanga kulifanya kuwa endelevu.Hersi alisema kuwa anaamini katika kikosi chao wapo baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao ipo mbioni kumalizika, hivyo kama wadhamini wamepanga kuhakikisha wanawabakisha kuendelea kukipiga Jangwani kwa lengo la kuiletea klabu mafanikio.

Aliongeza kuwa wachezaji hao watakaowabakisha ni wale wenye tija kwenye timu kwa kipindi chote walichoichezea Yanga bila ya kuangalia ukubwa wa jina lake.

“Huu mpango wa kuwaongezea mikataba tuliouanza tumepanga kuendelea nao siku za mbele ikiwa ni baada ya kumuongezea mkataba wa miaka miwili beki wetu, Lamine Moro.

“Moro tumemuongezea mkataba baada ya kutambua mchango wake katika timu, hicho kigezo tulichokitumia kwake ndiyo tutakavyotumia kwa wachezaji wengine kuwaongezea mikataba.

“Tulianza kwa Moro, hivyo wachezaji wengine wanafuatia hivi sasa uongozi unapitia mkataba wa kila mchezaji kwa yule ambaye unakaribia kumalizika kwa kufuata vigezo vyetu, basi tutamuongezea mwingine,” alisema Hersi.

Ikumbukwe kuwa, GSM katika usajili wa dirisha kubwa msimu huu, ilihusika kwa kiasi kikubwa kushusha nyota wapya ndani ya Yanga.

Miongoni mwa nyota hao ni Carlos Carlinhos raia wa Angola, Michael Sarpong (Ghana), Yacouba Songne (Burkina Faso), Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe ambao wote ni raia wa DR Congo.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad