Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Kocha Simba: Huyu Kaze Tumpe Muda tu

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURELIYEWAHI kuwa kocha na mchezaji wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amempa muda kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze kuweza kufanya vyema katika timu yake hiyo kutokana na tambo ambazo zimekuwa zikizungumzwa kuhusu kocha huyo.

Yanga imemshusha Kaze kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Kocha Mserbia, Zlatko Krmpotic kutokana na timu kushindwa kucheza soka la kuvutia licha ya kuwa alikuwa anapata ushindi.


 


Akizungumza na Championi Jumamosi, Julio alisema kuwa, ni mapema mno kuweza kumzungumzia Kaze kuwa atafanya nini katika kikosi hicho kwa kuwa makocha wengi wamekuwa wakitua kwa mbwembwe kisha kutimuliwa.


 


“Nimeweza kuisikiliza vizuri historia ya Kaze, ni kocha anayesifika kufanya vizuri, lakini ni mapema mno kuweza kumpa alama hadi atakapoanza kazi na kuona uwezo wake katika kikosi hicho na kuisaidia timu yake ya Yanga.


 


“Ligi ina ushindani mkubwa, mara nyingi makocha wamekuwa wakitua katika kikosi cha Yanga na kupewa sifa ambazo si za kwao halafu mwisho wa siku wanafungashiwa virago vyao, hivyo ni vyema wakamuamini na kupewa nafasi ili aweze kuifanya kazi yake kiufasaha,” alisema Julio.

Post a Comment

0 Comments